*Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu Ulemavu na Afya 2023

Karibu Insight, jukwaa la kidijitali linalowakutanisha watu wenye uziwikutoona na wale wanaowapa usaidizi, kwa ajili ya kubadilishana maarifa, kujenga mahusiano na kuimarisha jamii.

Insight inatoa taarifa zinazopatikana kwa urahisi, mafunzo na maudhui ya vitendo yanayowasaidia watu wenye uziwikutoona na wale wanaowaunga mkono kuongeza uelewa na maarifa, kushiriki kikamilifu na kustawi katika jumuiya zao, pamoja na kujenga mahusiano na ulimwengu unaowazunguka.

Ikiwa imeandaliwa kwa kushirikiana na watu wenye uziwikutoona, Insight inavuka mipaka ili kuhakikisha kuwa watu wenye uziwikutoona hawaachwi nyuma kadri dunia yetu inavyozidi kuwa ya kidijitali.


Kuwasaidia watu wenye uziwikutoona kuishi, kujifunza na kustawi. 

Nakala ya Hotuba

Maelezo: Video hii imetolewa na Sense International Kenya, na hotuba inatolewa na Julius Muga Ogayo, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Advocacy Against Discrimination of Disabled Kenya (AADD-Kenya) na Mjumbe wa Bodi ya Sense International Kenya. Kamera inaanza ikimlenga Julius, mwanaume mweusi aliyevalia suti ya buluu, shati jeupe na tai yenye mistari, akiwa katika ukumbi wa tukio wenye bango na nembo ya Sense International nyuma yake.

Katika hotuba yote, picha kutoka kwa timu za Sense International katika nchi mbalimbali zinaonekana kwenye skrini huku sauti ya Julius ikiendelea kusikika. Mwishoni mwa hotuba, kamera inamrejea Julius anapokamilisha ujumbe wake.

Julius:

Ujumuishaji wa kidijitali si chaguo tena; ni hitaji la msingi, ni tegemeo la maisha.

Katika dunia ya leo, upatikanaji wa teknolojia ya kidijitali ni ufunguo wa kupata elimu, ajira, huduma za afya na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiraia.

Bila upatikanaji huo, watu hubaki nyuma.

Kwa watu wenye uziwikutoona na ulemavu wa hisia nyingi, teknolojia za kidijitali zinaweza kuwa tofauti kati ya ukimya na mawasiliano, kati ya kutengwa na kushiriki, na kati ya utegemezi na kujitegemea.

Teknolojia hubadilisha upweke kuwa muunganiko, ukimya kuwa uwezo wa kujieleza, na kukata tamaa kuwa matumaini.

Watu wenye uziwikutoona wanaweza kujifunza, kufanya kazi na kushiriki kikamilifu katika jamii zao. Wanaweza kupata taarifa, kujieleza na kuchangia maendeleo ya jamii kwa usawa na wengine. Huu ndio uwezo wa ujumuishaji wa kidijitali na hiki ndicho Sense International inachokifanya.

Kwa hiyo, kitovu hiki cha rasilimali si jukwaa tu; ni tamko kwamba ujumuishaji unawezekana, kwamba teknolojia inaweza kuziba pengo lililopo, na kwamba haki za watu wenye uziwikutoona zinapaswa kutambuliwa na kutekelezwa.

Tuimarishe ushirikiano wetu ili sauti za watu wenye uziwikutoona na watu wengine wenye ulemavu ziongoze kila suluhisho tunalobuni.

Asanteni.


Saidia kuanza 


Raslimali kwa ajili ya kufundishia, malezi, kujifunzia na kustawi 


Upendo wa Dipak wa kujifunza

A woman sat facing a young man with deafblindness using tactical sign language.

“Dipak anastahili kupata mazingira sawa ya kujifunza kama ilivyo kwa mtu mwingine, na kumwezesha kuendelea kustawi.”

Mwalimu wa Dipak

Jisajili ili upokee taarifa kuhusu Insight, rasilimali mpya na kazi yetu kuhusiana na uziwikutoona.